0
as_barkley
Manchester City watatakiwa kulipa ada ya uhamisho ambayo itakua ya kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza ya kiasi cha paundi milioni 60 kama watakua wanahitaji huduma za kiungo wa klabu ya Everton Ross Barkley. 

Klabu ya Manchester City imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo lakini klabu yake ya Everton ndio imeibuka kuwa tatizo kutokana na matakwa yao hayo ya ada kubwa ya uhamisho wa rekodi wanayoitaka kutoka kwa matajiri hao wa jiji la Manchester.

Mwingereza Ross Barkley ametokea kuvivutia vilabu kadhaa vy nchini Uingereza zikiwemo  Manchester United na Chelsea lakini Manchester City wameibuka kuwa vinara wa mbio hizo na huenda wakamnyakua kiungo huyo mnamo mwezi January au mwishoni mwa msimu.

Bosi wa Everton, Roberto Martinez ametanabahisha kuwa kiungo wake Barkley bado yupoyupo sana mitaa ya Goodison Park na hatarajii kumuona akiondoka siku za hivi karibuni.

Lakini wadadisi wengi wa masuala ya soka nchini uingereza wanadai huenda mchezaji huyo akafuata nyayo za mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa anakipiga na mashetani wekundu wa Manchester United Wayne Rooney ambaye alilazimisha uhamisho wake wa kujiunga na mashetani wekundu hao mnamo mwaka 2004.

Post a Comment

 
Top