0
Issa Hayatou, president of CAF, held talks to try and save the 2015 Africa Cup of Nations. Photograph: Fadel Senna/AFP/Getty Images
Morocco imelikatalia katakata shirikisho la soka barani Africa CAF kuandaa mashindano ya Mataifa ya Africa mnamo mwezi January mwakani hofu ikiwa uwezekano wa kusambaa kwa virusi vya maradhi yanayoutikisa ulimwengu kwa sasa ya Ebola. 

Serikali ya Morocco ililiomba shirikisho hilo kuyasogeza mbele mashindano hayo yaliyopangwa kuanza kushika kasi mnamo January 17. Katika taarifa yake hiyo CAF walithibitisha kuwa wao watakua tayari kuyasogeza mashindano hayo kutoka tarehe tajwa hapo juu kwenda February 8 mwakani jambo ambalo limekataliwa na shirikisho hilo la soka barani Africa.

Taarifa ya serikali iliyotolewa na Waziri wa Michezo wa nchini Morocco ilisema: “Maamuzi haya yanatokana na tishio la maradhi ya Ebola na kusambaakwake." 


Post a Comment

 
Top