0
View image on Twitter

Kikundi cha mashabiki wa klabu ya Liverpool wamepanga kufanya kile kilichowahi kufanywa na mashabiki wa watani wao wa jadi Manchester United kwenye harakati zao za kumng'oa David Moyes na mpango wao wa kumrejesha mshambuliaji Cristiano Ronaldo pale ambapo waliamua kurusha ndege ndogo ikiwa na mabango yenye ujumbe tofauti.

 Rodgers is set to rest Gerrard against Real Madrid and start Henderson as captain for Liverpool on Tuesday

Mashabiki hao wa Liverpool wanaohitaji mwalimu Brendan Rodgers atimuliwe kutokana na matokeo mabovu ya siku za karibuni ya mabingwa hao mara 19 wa ligi kuu nchini Uingereza.Mashabiki hao wanaoonekana kukata tamaa na matokeo ya Liverpool wamepanga kulirusha bango hilo siku ya Jumapili wakati timu hiyo itakapokuwa ikikipiga dhidi ya matajiri wa jiji la London klabu ya Chelsea iliyoko kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.


Manager Rodgers is making a big call to rest a man with 70 Champions League appearances to his name

Mashabiki hao wanaonekana kutokuwa na imani na mfumo wa usajili wa Rodgers kutokana na kitendo chake cha kuwanyakua wachezaji wengi kutoka kwenye klabu ya Southampton na wanamuona kama bado ni mshabiki wa klabu yake ya zamani aliyokuwa akiifundisha ya Swansea na wanamchukulia pia kama mfujaji kwa matumizi yake ya jumla ya paundi milioni 215 kuwa ni matumizi mabovu ya pesa tena yasiyo na tija ndani yake.

Post a Comment

 
Top