0

Fellaini was seen as a scapegoat for David Moyes' (right) poor spell as United managerKiungo wa klabu ya Manchester United Marouane Fellaini amezungumza mbele ya waandishi wa habari na kutoa maneno mazito sana ya moyoni kwa mashabiki wa timu hiyo waliokuwa wakimuona yeye kama mbuzi wa kafara kutokana na matokeo mabovo ya msimu uliopita ya klabu hiyo chini ya David Moyes.

Fellaini alikua mchezaji pekee aliyesajiliwa na Meneja aliyetimuliwa mara baada ya msimu mmoja tu David Moyes mnamo mwaka 2013 kwenye majira ya usajiri ya kiangazi kwa ada inayokisiwa kuwa ni paundi za Uingereza milioni 27.5 akitokea klabu ya Everton.

 The big midfielder is yet to return to the form which made him such a key player for Everton
Alipoulizwa kama yeye alikua ni mbuzi wa kafara kwenye msimu huo mbovu kabisa kwa klabu hiyo Fellaini alisema: "Ndio kwa kiasi fulani. Hilo ni swali gumu kidogo, Ambalo ni gumu kidogo kulijibu, Sikukata matumaini licha ya kuwa mazonge yalikua mengi sana dhidi yangu kwani niliandamwa nikiwa uwanjani na nje ya uwanja lakini kibaya zaidi ni kuandamwa ndani ya mitandao ya kijamii, iliniumiza sana japo nilijipa moyo wa kijasiri wa kupambana."

 The 26-year-old impressed as Louis van Gaal's side held Premier League leaders Chelsea at Old Trafford
"Familia yangu ilinisaidia sana kuweka sawa hali ya mambo ilivyokua ikiendelea kwa wakati ule, Lakini kumbukeni kuwa kwa wakati ule nilikuwemo pia kwenye kikosi cha timu ya Taifa langu kwaajili ya michuano ya kombe la Dunia na namshukuru Mungu nilicheza vizuri halikadhalika kwa timu yangu pia hivyo nikarejea tena kwenye majukumu yangu ya klabu nikiwa na imani na matumaini tele kutokana na kiwango changu kuimarika."

Fellaini believes an impressive World Cup campaign with Belgium has put him in good shape for the season
"Nilipofika hapa nilikutana na jambo jingine tena ambalo lilinifanya nichanganyikiwe zaidi pale meneja aliponiambia kuwa kama ninahitaji kubakia ndani ya klabu basi ninahitaji kupambana sana kwani mimi ni mmoja kati ya wachezaji ambao sikuwemo kwenye mipango yake ndani ya klabu."

 The Belgian midfielder seems to be flourishing under the guidance of United boss Van Gaal
"Sikukata tamaa nimejitahidi kujiimarisha na kurejea katika kiwango changu lakini kwa ujumla miongoni mwa kitu kinachonipa faraja zaidi kwa sasa ni kurejeshwa kwenye eneo langu asilia la majukumu yangu uwanjani hivyo natarajia kuona sifa nyingi sana nje na ndani ya uwanja kutoka kwa mashabiki walewale waliokuwa wakiniona sina tija ndani ya kikosi,kuniona mbuzi wa kafara na ninaimani wataniandika vyema kwenye mitandao yao ya kijamii pia."

Post a Comment

 
Top