0
Wenger refuses to comment on Arsenal fans' banner urging him to leave
Licha ya ushindi wa goli 1:0 walioupata siku ya jana kwenye dimba la  The Hawthorns dhidi ya klabu ya West Brom mashabiki wa klabu ya Arsenal wameshindwa kuzizuia hisia zao zinazomtaka Mfaransa Arsene Wenger kuiachia timu hiyo licha ya kukubali kuwa katika kipindi chote ambacho wamekua nae amewatendea mazuri mengi pia.

Mara baada tya kipyenga cha mwisho kupulizwa mashabiki hao wa klabu ya Arsenal walilionesha bango kubwa lililokuwa na maandishi ya kumshukuru mfaransa huyo lakini wakimtaka kuondoka klabuni hapo ikiwa ni ishara ya kuchoshwa na mwenendo wa timu hiyo kwa sasa.

Danny Welbeck alifunga Arsenal goli pekee lililoipatia alama tatu muhimu klabu ya hiyo iliyo katika mbio za kutaka kunyakua ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.

Bango hilo lilisomeka: ‘Arsene. Thanks for the memories but it’s time to say goodbye.’ likimaanisha kumshukuru Wenger kwa yote mazuri aliyoifanyia klabu hiyo lakini likimtaka pia kuangalia ustaarabu mwingine na kuiacha klabu hiyo chini ya utawala mwingine.

Bosi huyo wa klabu ya Arsenal alipoulizwa baadae kwenye masaili baada ya mchezo huo aligoma kuzungumzia jambo lolote kuhusiana na kipeperushi hicho licha ya waandishi kumlazimisha kutoa maoni yake kuhusiana na bango hilo.

Walipomlazimisha sana kutoa maoni yake juu ya suala hilo mzee Wenger alisema "Sihitaji kulizungumzia suala hilo kwa sasa kwani kazi ya umeneja wa klabu hiyo si kwaajili yangu tu bali kwaajili ya mtu yeyete yule anayekidhi vigezo vya wamiliki wa timu hiyo"

Post a Comment

 
Top