0
Chelsea fan sells his car to buy pricy tennis tickets near Mourinho
Shabiki mmoja wa klabu ya Chelsea amejikuta akiuza gari yake ili apate pesa ya kununulia tiketi ya daraja la juu ya kushuhudia michuano ya tennis ya ATP World Tour lakini lengo mahususi la kukata tiketi hiyo likiwa ni kuhakikisha anakaa karibu na bosi wa the Blues, Jose Mourinho.

The Special One alihudhulia mchezo huo kwa malengo ya kumpatia ushauri wa kiufundi Mwingereza Andy Murray aliyekua akimenyana na Muhispania Roger Federer.

Kwenye mchezo huo maneno ya kocha huyo msema hovyo aliyomnasihi mcheza tenesi huyo hayakufua dafu kwani mpaka mwisho wa mchezo huo Murray alipoteza mchezo huo mbele ya Federer.

Kukaa kwenye jukwaa hilo maalumu kumemfanya shabiki huyo kupoteza gari lake lakini angalau alijifariji kwa kukaa sehemu ambayo walikua wakinyang'anyana hewa ya Oksijeni na mtu maarufu kama Morinho.

Post a Comment

 
Top