Mshambuliaji huyo wa klabu ya Manchester United amekanusha taarifa hizo zilizozagaa miongoni mwa vyombo vingi vya habari Ulimwenguni kuhusiana na tiba hiyo mbadala anayoitumia Radamel Falcao kililinda jeraha lake hilo lililomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Ikumbukwe kuwa mshambuliaji huyo amekwisha tumia miezi kadhaa kuliuguza jeraha lake hilo lililomfanya ayakose mashindano ya kombe la Dunia nchini Brazil, jeraha ambalo alilipata wakati akikitumikia klabu chake cha AS Monaco mnamo mwezi January mwaka huu.
Taarifa za kitabibu kutoka ndani ya klabu ya Manchester United zianadai kuwa kulifunga jeraha hilo kwa barafu ni moja kati ya tiba mbadala ambazo ni lazima kufanywa ikiwa ni moja kati ya njia ya kuweza kulizui jeraha hilo lisiendelee kuleta madhara zaidi na hivyo kukanusha taarifa zilizokua zikidai kuwa mshambuliaji huyo huwa anafanya hivyo ili kujitibu kutokana na jeraha hilo kuanza kumsumbua tena na hivyo kudai kuwa huo ni uzushi na uongo unaoenezwa na watu ambao sio wakweli na waliojawa na uzushi pia.



Post a Comment