0
Equatorial Guinea to host Africa Cup of Nations
Shirikishola soka barani Afrika CAF limethibitisha rasmi kuwa nchi ya Equatorial Guinea ndiyo itakayokuwa mweneji wa michuani ya Afrika mnamo mwaka 2015 mara baada ya Morocco kujitoa dakika za mwisho kwenye jukumu la kuandaa fainali za mashindano hayo.

Morocco iliyokabidhiwa jukumu na CAF la kuandaa fainali za michuano hiyo ililiomba shirikisho hilo kusogeza mbale muda wa kuanza kwa mashindano hayo kutokana na hofu iliyotanda ya mlipuko wa virusi vya ugojwa hatari  wa Ebola unaotajwa kuwa tayari umekwisha sababisha vifo vya zaidi ya watu 5000 barani Afrika ombi ambalo lilitupiliwa mbali na shirikisho hilo na sasa kuwazawadia Equatorial Guinea nafasi ya kuandaa mashindano hayo. 

Kwa mujibu wa raisi wa shirikisho hilo Issa Hayatou amesema kuwa katika kikao chao cha dharula kilichofanyika hii leo wameamua kuipa jukumu hilo nchi ya Equatorial Guinea ambayo imeiagiza kutumia viwanja vyake vya kwenye miji ya Malabo, Bata, Mongomo na Ebebiyin.

"Raisi wa Jamuhuri ya watu wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ameupokea ujumbe wa CAF kutoka kwa raisi wake Issa Hayatou hii leo kuhusiana na maombi ya shirikisho hilo kulitaka taifa lake kuandaa mashindano hayo na tayari amekwisha kubali kuandaa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo January 17 mpaka February 8 mwaka 2015 kwenye miji tajwa hapo juu.

"Kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika CAF ikiongozwana raisi wake Issa Hayatou inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa raisi mteule wa Jamuhuri ya watu wa Equatorial Guinea mheshimiwa Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, Serikali yake na chama cha soka cha Equatorial Guinea kwa kukubaliana na maombi yetu haya ya ghafla."Taarifa ya CAF ilisema.

Nchi ya Equatorial Guinea pia imetajwa kuwa mbadala wa  Morocco miongoni mwa timu zitakazoshiriki michuano hiyo licha ya kuwa awali ilishindwa kufuzu kwaajili ya michuano hiyo pale ambapo CAF iliinyang'anya ushindi kutokana na nchi hiyo kumchezesha mchezaji ambaye si halali.

Post a Comment

 
Top