0
Wenger responds to Campbell loan move claims
Bosi wa klabu ya washika mitutu wa Emirates Mfaransa Arsene Wenger amemwambia mshambuliaji wake kuwa ananafasi ya kuendelea kung'ara ndani ya klabu hiyo lakini si sasa kwani kwa sasa haioni nafasi yake yeye ndani ya klabu hiyo na hivyo kumwambia kuwa anaweza kwenda kokote atakako ila kwa mkopo na si kuuzwa moja kwa moja.

Campbell tayari amekwisha vitumikia vilabu kadha wa kadha kwa mkopo kwa misimu mitatu tofauti tangu alipojiunga na klabu ya Arsenal. Mara baada ya kuonesha kiwango cha juu akiwa na timu yake ya Taifa kwenye michuano ya Kombe la dunia Campbell alikua anatarajia kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Wenger jambo ambalo limekua kinyume na matarajio yake. 

Campbell amecheza michezo miwili tu ya Premier League msimu huu na wadadisi wa masuala ya soka wanadai kuwa huenda mchezaji huyo akaondoka kwa mkopo mnamo mwezi January mwakani.a

Vilabu vya AC Milan, Galatasaray na Olympiakos vyote kwa nyakati tofauti vimeonesha nia ya kutaka kumsajili Campbell.

Post a Comment

 
Top