Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Guus Hiddink ametanabahisha kuwa atajiuzuru katika nafasi yake hiyo ya ukocha iwapo tu atapoteza mchezo ujao dhidi ya timu ya Taifa ya Latvia unaotarajiwa kuchezwa wiki ijayo kwaajili ya kufuzu kwa michuano ya Ulaya ya mwaka 2016.
Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea aliyeshika nafasi ya Louis van Gaal
mara baada ya michuano ya World Cup, nchini Brazil na sasa anaonekana kukalia kuti kavu kutokana na ukweli kwamba tayari amekwisha poteza mchezo dhidi ya jamuhuri ya Czech na Iceland na kuifanya timu yake mpaka sasa kushikiria nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi A.
Kocha huyo aliyeiwezesha timu ya Korea Kusini kufikia hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la Dunia mnamo mwaka 2002 amethibitisha kuwa ataachana na nafasi hiyo iwapo tu atapoteza mchezo ujao dhidi ya Latvia unaotarajia kuchezwa kwenye dimba la Amsterdam Arena hapo November 16.
Hiddink amewajumuisha kikosini walinzi Jetro Willems na
Ricardo van Rhijn wa klabu ya PSV Eindhoven na Ajax. Pia mlinzi wa klabu ya Aston Villa Ron Vlaar anatarajiwa kurejea tena kikosini mara baada ya kukosa michezo ya awali kutokana na maumivu.Lakini pia katika kikosi chake hicho amewatema viungo wa klabu ya QPR Leroy
Fer na Virgil van Dijk.
Kikosi kamili cha Hiddink alichokiita kwaajili ya mchezo huo ni:-
Walinda Mlango: Jasper Cillessen (Ajax), Tim Krul (Newcastle United), Kenneth Vermeer (Feyenoord)
Walinzi: Bruno Martins Indi (FC Porto),
Joel Veltman (Ajax), Ricardo van Rhijn (Ajax), Ron Vlaar (Aston Villa),
Stefan de Vrij (Lazio), Gregory van der Wiel (Paris Saint-Germain),
Jetro Willems (PSV)
Walinzi: Ibrahim Afellay (Olympiakos),
Daley Blind (Manchester United), Jordy Clasie (Feyenoord), Nigel de Jong
(AC Milan), Davy Klaassen (Ajax), Wesley Sneijder (Galatasaray),
Georginio Wijnaldum (PSV)
Washambuliaji: Memphis Depay (PSV), Klaas-Jan
Huntelaar (Schalke), Luciano Narsingh (PSV), Robin van Persie
(Manchester United), Quincy Promes (Spartak Moskow), Arjen Robben
(Bayern Munich)
Post a Comment