Kiungo raia wa Brazil anayekipiga ndani ya klabu ya Chelsea, Oscar amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya darajani utakaomfanya kubakia darajani mpaka mwaka 2019.
"Nafurahia kukipiga ndani ya klabu ya Chelsea kwa miaka miwili niliyokaa hapa na sasa nina miaka mitano zaidi ya kuwepo hapa ninafuraha sana kuwa mmoja kati ya wanafamilia hii yenye upendo" Oscar aliuambia mtandao wa klabu Chelsea.com.
Oscar aliyekuwemo kwenye kikosi cha Brazili kilichoshindwa kufanya vyema kwenye michuano ya ya kombe la Dunia lililofanyika kwenye ardhi ya nyumbani kwao mwaka huu tayari amekwisha ichezea Chelsea jumla ya michezo 92 na kufanikiwa kuifungia takribani magoli 27.
Post a Comment