Katika hali inayoonesha kama kukumbwa na jinamizi la mkosi ndani ya klabu ya Manchester United kushika hatamu imeripotiwa kuwa golikipa namba moja wa timu hiyo David De Gea
atatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne (mwezi mmoja) baada ya kuumia kidole akiwa mazoezini na timu yake ya taifa ya Hispania.
Golikipa huyo wa klabu ya Manchester United amefanyiwa uchunguzi siku ya jana na Daktari wa timu ya taifa ya Hispania ambaye mara baada ya uchunguzi huo amethibitisha kuwa itamlazimu nyanda huyo kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja ili kupona kabisa jeraha lake hilo.
Golikipa huyo ambaye anatajwa kuwa na msimu mzuri sana pale United msimu huu ameyatwaa majeraha hayo alipokua akijaribu kuliokoa shuti dhaifu lilipigwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Hispania Paco Alcacer wakiwa mazoezini kujiandaa kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Belarus mjini Huelva.
De Gea anaungana na wachezaji wenzake Cesc fabregas na Diego Costa kwenye orodha ya majeruhi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambapo imearifiwa kuwa Fabregas anasumbuliwa na tatizo la misuli ya paja.
'Mlinda mlango David de Gea amelazimika kusitisha mazoezi mara baada ya kuumia kidole kidogo cha mwisho cha mkono wake wa kulia,' Taarifa imeandikwa kwenye tovuti ya chama cha soka cha mchini Hispania.
Maumivu haya yanakua kama mkosi kwa mlinda mlango David De Gea, ambaye kwa siku za hivi karibuni amekua akianza kuaminika kuchukua mikoba ya mlinda mlango mkongwe wa timu ya Real madrid na timu ya taifaya Hispania Iker Casillas kama mlinda mlango namaba moja.
Maumivu haya ya De Gea ni pigo kubwa kwa meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ambaye tayari amekwishakuwa na lundo la majeruhi kwa wachezaji wake wa safu ya ulinzi na sasa anatarajiwa kumkosa amlinda mlango wake namba moja kwa wikikadhaa.
Van Gaal sasa atakua na jukumu la kuamua kuwatumia kati ya mlinda mlango namba mbili wa timu hiyo Anders Lindegaard,
ambaye tayari mwanzoni mwa msimu huu alikwishaambiwa kuwa anaweza kutafuta timu atakayokuwa na nafasi ya kucheza au kumpa nafasi mlinda mlango chipukizi wa timu hiyo anayedakia timu ya taifa ya Uingereza kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 21 Ben Amos.
Mlinda mlango wa zamani wa klabu ya
Barcelona, Victor Valdes amekua akifanya mazoezi na klabu ya Mancester United kwa siku kadhaa ikiwa ni mazoezi yake ya mwanzomwanzo tangu arejee kutoka kwenye maumivu ya mguu yaliyomuweka nje ya uwanja kwa takribani nusu msimu sasa.
Post a Comment