Mikel Arteta amekubali kusaini mkataba utakaomfanya kuendelea kubakia kwa mwaka mmoja zaidi na washika mitutu wa jiji la London klabu ya Arsenal. Mkataba huo aliousaini mchezaji huyo huenda ukaongezwa kwa mwaka mmoja zaidi endapo tu ataonesha kiwango kinachomvutia meneja wa timu hiyo Mfaransa Arsena Wenger.
Arteta amekua kwenye mazungumzo ya makubaliano ya mkataba mpya na The Gunners kwa muda mrefu sasa ili na yeye ajumuishwe kwenye orodha ya wachezaji walioongezewa mkataba na klabu hiyo huku mashabiki wengi wa klabu hiyo wakiw a wameshikwa na kizungumkuti kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu ulivyoporomoka kwa siku za hivi karibuni.
Taarifa zilizotolewa na mtandao wa Goal.com zinasema kuwa veterani huyo sasa amefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi na huenda akaongezewa mwaka mmoja zaidi iwapo tu atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha washika mitutu hao wa jiji la London.
Mkataba wa awali wa Mikel Arteta ulikua ukimalizika mnamo mwishoni mwa msimu huu na alikua akihusiswa na kujiunga na vilabu kadhaa vya nchini Italia na Uhispania.
Taarifa za kuaminika kutoka katika moja ya vyanzo vya uhakika vya habari ndaji ya klabu hiyo zinadai kuwa Arteta ameongezewa pia masilahi yake ikiwa ni sehemu ya kumshawishi kiungo huyo kubakia na timu.
Post a Comment