Cristiano Ronaldo Usiku wa jana aliandikisha rekodi mpya ya kihistoria katika harakati za kufuzu kaajili ya michuano ya Ulaya mara baada ya kuifungia timu yake ya taifa tya Ureno goli moja na la pekee na hivyo kuwa ndiye mfungaji anyeshikiria rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye hatua hiyo ya awali.
Goli hilo la peke la Ronaldo kwenye mchezo huo dhidi ya timu ya taifa ya Albania limemfanya mshambuliaji huyo kuandikisha historia hiyo mpya na kuendelea kuwa na wakati mzuri wa kuendele kuandikisha rekodi mbalimbali katika tasnia ya mpira wa miguu barani Ulaya na Duniani kwa ujumla.
Seleccao walionekana kubanwa sana kwenye mchezo wa jana lakini juhudi binafsi za nahodha wao huyo Cristiano Ronaldo zilikuja kuzaa matunda mnamo dakika ya 72 mara baada ya kumalizia nafasi nzuri iliyotengenezwa na Luis Nani na kuipeleka timu yake kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi I nyuma ya timuya taifa ya Denmark.
Kwa goli hilo sasa Ronaldo anasogea mpaka nafasi ya kwanza akiwa na magoli 23 akiwapita mchezaji wafuatao ambao wengi wao tayari wamekwishaachana na soka la kimataifa.
1. John Dahl Tomasson. (Denmark/Magoli 22)
2. Robbie Keane. (Ireland/Magoli 21)
3. Jan Koller.(Czech/Magoli 21)
4. Hakan sukur.(Uturuki/Magoli 21)
Post a Comment