0
Inter sack head coach Mazzarri 
Klabu ya Inter Milan ya nchini italia hii leo imevunja mkataba na kocha aliyejiunga na timu hiyo miezi 17 iliyopita Walter Mazzarri kufuatia kile wanachokidai mabosi hao wa klabu hiyo kuwa ni mwenendo mbaya wa klabu hiyo kwa sikuza hivi karibuni na wamemtaja meneja wa zamni wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini kuwa mbadala wake.

Mazzari mwenye umri wa mika 53 alijiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 2013 akitokea kwenye klabu ya Napoli ambako alifanya vizuri sana. 
 Mancini (left) gets to grips with Balotelli during a heated training session in 2013

Mabosi hao wamedai kuwa wao kama wamiliki wa timu hiyo walikua na matumaini makubwa sana na kocha huyo ambaye alikua na matokeo ya kuvutia sana alipokuwa na Napoli kitu ambacho ameshindwa kukipeleka ndani ya Giuseppe Meazza kwani msimu wake wa mwanzo tu ilishuhudiwa akimaliza katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi hiyo na hivyo kuipoteza nafasi adhimu ya kushiriki michuano ya Champions League.

Mabosi hao wamedai kuwa wanamuona Mazzarri kama ni mtu aliyeshindwa kazi kwani mpaka sasa timu hiyo inashikiria nfasi ya 9 baada ya michezo 11 ya ligi iliyocheza.

"FC Internazionale Milan inatangaza kuwa meneja Walter Mazzarri amesitishiwa mkataba wake wa kuwa mwalimu wa kikosi cha kwanza cha timu hii, Klabu inapenda kumshukure Mazzari kutokana na uwajibikaji wake na kujitolea kwake kuhakikisha kuwa Inter inafikia katika kilele cha mafanikio katika miezi 17 yake yote aliyokuwa hapa kama kocha wetu" Taarifa ya klabuhiyo ilisema

Roberto Mancini si mgeni ndaniya klabu ya Inter Milan kwani tayari amekwisha wahi kufanya kazi hapo kwenye msimu wa 2004-2008 na kuiongoza vyema timu hiyo kutwaa mataji matatu ya Serie A na mawiliya Coppa Italia kabla ya kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na msema hovyo Jose Morinho, Mancini  anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa kocha wa Inter Milan na mmiliki wa klabu hiyo Erick Thohir kama mrithi wa Mazzarri.

Post a Comment

 
Top