0
Sanchez was the star man in the Premier League match at the Emirates at the weekend
 
Mshambuliaji Alexis Sanchez ameendelea kuthibitisha ubora wake mara baada ya kuifungia timu yake ya Arsenal magoli mawili na kuisadia kuibuka na ushindi wa jumla wa magoli 3:0 dhidi ya  Burnley. 
 
Nijuavyo mimi Alexis Sanchez ni mmoja kati ya washambuliaji wenye tabia ya kujitolea na kupambana kwaajili ya timu yake akitegemea zaidi ubora, na kipaji kikubwa cha kusakata kabumbu alichonacho kitu ambacho si kila mcheza mpira anacho.

Tangu mzee Wenger aamue kumtumia kama mshambuliaji wa kati Sanchez ametokea kuwa mshambuliaji hatari zaidi katika suala la kufumania nyavu na siku za hivi karibuni kuuteka upepo wote uliokuwa ukivuma kuelekea kwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa huku siraha kubwa anayoonekana kuitumia Sanchez ni kujiamini, nguvu na kujiweka katika mahala muafaka kwaajili ya kuyatekeleza majukumu yake ya kutupia kambani (kwenye njia za mipira)

Rekodi ya Ufungaji wa Magoli ya Mshambuliaji Alexis Sanchez katika vilabu mbalimbali alivyowahi kuvichezea.

Klabu Michezo Magoli Pasi za mwisho
Arsenal
15
10
3
Barcelona
141
47
36
Udinese
112
21
20

Post a Comment

 
Top