Clabu ya Real Madrid inamsaka kwa udi na uvumba kiungo wa pembeni wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Eden Hazard ili akawe mbadala wa winga Gareth Bale ambaye amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara yanayomfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake yanayomfanya awe ndani ya Madrid.
Licha ya maumivu hayo ya mara kwa mara lakini kitendo cha Mashetani wekundu wa Manchester United kutangaza hadharani kuwa watatuma ofa ya paundi milioni 90 kwa klabu ya Real Madrid ili kumnasa mshambuliaji huyo wa Wales kinawafanya Madrid kuanza kuhaha kumtafuta mbadala wa mshambuliaji huyo.
Kutokana na mazingira hayo Real imeamua kuanza kujipanga mapema kutafuta suluhisho la tatizo linalotarajiwa kuwakumba hivyo Hazard ndiye atakayekuwa mbadala sahihi kwa nafasi hiyo endapo tu Bale ataamua kurejea kwenye Premier League.
Post a Comment