Arsenal inaelekea kwenye mchezo wao wa UEFA Champions League dhidi ya Anderlecht ikiwa na kumbukumbu za ushindi katika mechi zilizopita za Premier League.
katika michezo hiyo iliyopita The Gunners wameonekana kuimarika sana katika idara mbalimbali na sasa wananafasi kama hiyo ili kuudhihilishia umma wa wapenda soka katika kuhakikisha wanapata ushindi wa tatu mfululizo wa michuano hiyo siku ya kesho.
Ili kukamilisha mpango huo mimi natamani sana kumuona mzee Wenger akifanya mabadiliko haya madogo kwenye kikosi chake cha kwanza.
1) Aaron Ramsey badala ya Mikel Arteta.
Arsenal ilifanikiwa kuutawala mchezo dhidi ya Burnley, lakini iliwalazimu kutumia dakika takribani 30 kupata goli la kuongoza mara baada ya Ramsey kuchukua mahala pa Arteta.
Ramsey hakuhusika katika goli lolote lile kati ya magoli yote mawili ya Arsenal lakini kikubwa alichokifanya kwenye mchezo huo ni kuifanya sehemu ya ulinzi ya Burnley kuanzakutafuta njia mbadala ya kukabiliana na mishemishe za kiungo huyo mkabaji.
Kinachonifanya nimtamani sana Ramsey kwenye mchezo huo ni kwa sababu tu Arsenal wanahitaji kushambulia sana kwenye mchezo dhidi ya Anderlecht kuliko kujilinda zaidi jambo ambalo litakua ni la hatari sana kwa upande wa klabu hiyo kuliko kuwatumia viungo watakaokuwa wanakaa sana nyuma na kujaribu kuwakera wapinzani wao kwa kuwatibulia mipango tu.
Sioni umuhimu wa uwepo wa Arteta na Mathieu
Flamini kuelekea mchezo huo katika sehemu ya kiungo kutokana na ukweli kwamba viungo hawa wataisaidia zaidikwenye suala la kukaba na si kushambulia.
2. Lukas Podolski badala ya Santi Cazorla
Mimi sio shabiki mkubwa wa Lukas Podolski, lakini wakati Cazorla anapocheza kama alivyocheza kwenye mchezo dhidi ya Burnley ni vigumu sana kutamani kumuona mtu kama yeye anakua kwenye kikosi cha kwanza na itakua sio halali kumuona Mjerumani huyo akiwa katika benchi kwenye mchezo mwingine tena na akiwekwa benchi na mtu wa kalba ya Cazorla.
Cazorla alishindwa kabisa kuonesha madhara kwenye mchezo huo akionekana kushindwa kuzitumia nafasi kadhaa alizozipata kwenye mchezo huo. Lakini muda mfupi alioupata Podolski aliweza kuzikosa zafasi mbili za wazi amabazo zote mashuti yake makali yaligonga miamba na kutudi uwanjani.
Mchezo huu ni lazima Arsenal washambulie kwa nguvu kwakuwa ukiachilia mchezo huo pia kwenye kundi lao kuna mchezo mwingine kati ya Galatasaray na Borussia Dortmund na kama Galatasaraya watapata matokeo dhidi ya BvB basi Arsenal huenda wakakosa nafasi kutokana na kupoteza mchezo wao wa mwanzo wa ufunguzi wa michuano hii na hivyo ikiwa michezo imesalia mitatu basi angalau Arsenal ijihakikishie nafasi ya kufuzu.
Post a Comment