Mara baada ya Meneja
wa klabu ya Manchester United Mholanzi Louis
van Gaal kuthibitisha maumivu ya mlinzi wake wa kati raia wa Argentina
Marcos Rojo ambaye amepata maumivu ya bega lake kwenye mchezo ambao
timu yake ilipoteza kwa goli 1-0
dhidi ya Manchester City kwenye dimba la Etihad.
Rojo
alitolewa mapema kipindi cha pili na kuwekewa mtungi wa gesi ya
oksijeni mara baada ya kupatwa na maumivu hayo ya bega kwenye mchezo
huo.
Muajentina huyo sasa ataungana na majeruhi wengine ndani ya klabu hiyo wakiwemo Rafael na Phil Jones na kutimiza idadi ya majeruhi takribani 35 ndani ya msimu mmoja.
Muajentina huyo sasa ataungana na majeruhi wengine ndani ya klabu hiyo wakiwemo Rafael na Phil Jones na kutimiza idadi ya majeruhi takribani 35 ndani ya msimu mmoja.
Orodha kamili ya wachezaji waliokumbwa na maumivu ndani ya msimu huu tangu Mholanzi Luis van Gaal achukue jukumu la kuwanoa mashetani wekundu hao ni:-
Jina la Mchezaji | Aina ya Maumivu | Tarehe aliyoumia |
---|---|---|
Michael Carrick | Mguu | 15th July 2014 |
Anderson | Nyonga | 17th July 2014 |
James Wilson | Dole gumba. | 18th July 2014 |
Rafael | Nyonga. | 25th July 2014 |
Chris Smalling | Nyonga | 29th July 2014 |
Danny Welbeck* | Kifundo cha Mguu. | 2nd August 2014 |
Antonio Valencia | Mguu. | 5th August 2014 |
Jonny Evans | Nyonga. | 5th August 2014 |
Luke Shaw | Misuli. | 7th August 2014 |
Jesse Lingard | Kifundo cha mguu | 16th August 2014 |
Marouane Fellaini | Mguu | 19th August 2014 |
Ander Herrera | Mguu. | 21st August 2014 |
Chris Smalling | Nyonga. | 24th August 2014 |
Shinji Kagawa* | Nyonga | 26th August 2014 |
Angel di Maria | Misuli | 30th August 2014 |
Juan Mata | Nyama za paja. | 30th August 2014 |
Phil Jones | Misuli. | 8th September 2014 |
Ashley Young | Kifundo | 9th September 2014 |
James Wilson | Kifundo | 9th September 2014 |
Jonny Evans | Mguu. | 21st September 2014 |
Chris Smalling | Nyama za paja. | 24th September 2014 |
Ander Herrera | Mbavu kupasuka | 27th September 2014 |
James Wilson | Mguu. | 29th September 2014 |
Radamel Falcao | Misuli | 5th October 2014 |
Paddy McNair | Misuli | 5th October 2014 |
Luke Shaw | Kifundo cha Mguu | 5th October 2014 |
Antonio Valencia | Misuli | 5th October 2014 |
Ander Herrera | Misuli | 20th October 2014 |
Angel di Maria | Nyonga | 20th October 2014 |
Phil Jones | Kifundo | 22nd October 2014 |
Ashley Young | Kifundo cha mguu. | 23rd October 2014 |
Radamel Falcao | Nyonga. | 24th October 2014 |
Wayne Rooney | Kifundo cha mguu | 27th October 2014 |
Rafael | Mguu. | 30th October 2014 |
Marcos Rojo | Bega. | 2nd November 2014 |
*Danny Welbeck na Shinji Kagawa wote wameondoka ndani ya klabu ya Manchester United mwanzoni mwa msimu huu.
Post a Comment