0
as_balotelli_ita
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mario Balotteli amefurahishwa na kitendo cha kujumuishwa tena kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Italia kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya ya mwaka 2016 dhidi ya Croatia.

Mshambuliaji huyo mwenye matata mengi nje na ndani ya uwanja hakusita kuionesha furaha yake hiyo pale alipoamua kuandika kwenye ukurasa wake rasmi wa facebook kuwa amefurahishwa sana na kuitwa huko “Ninafuraha kujumuishwa kwenye kikosi cha timu yangu ya taifa langu kwa mara nyingine tena, Na ninajivunia kuwa mwakilishi wa nchi yangu kuelekea kwenye mashindano hayo makubwa na muhimu kwa historia ya soka la nchi yangu ni fahari na heshima kubwa kuwemo kikosini,”

Hii ni mara ya kwanza kwa Super Mario kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia tangu kuisha kwa mashindano ya kombe la Dunia kule nchini Brazil katikati ya mwaka huu.

Post a Comment

 
Top