0
The Austrian international had set up the opening goal for Franck Ribery at the Allianz Arena 
Licha ya klabu ya Bayern Munich kufuzu kiurahisi kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League lakini gharama za kufuzu kwao ni kubwa sana kutokana na ukweli kwamba wanatarajiwa kuzikosa huduma za mlinzi wake wa pembeni raia wa Austria David Alaba kwa takribani miezi mitatu.

Alaba amepata maumivu ya kifundo cha mguu mnamo dakika ya 81 ya mchezo maumivu ambayo yatamfanya awe nje ya uwanja kwa miezi kadhaa. Uchunguzi wa awali uliofanywa na matabibu wa klabu ya Munich umetanabahisha kuwa mchezaji huyo amepata maumivu yatakayomfanaya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.


 Alaba joins a growing midfield injury list for the German champions

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Bayern zinadai kuwa uchunguzi zaidi unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa lakini tayari meneja wa timu hiyo amekwisha thibitisha kutozipata huduma za mchezaji huyo kwa takribani miezi mitatu.

Tayari klabu ya Bayern inazikosa huduma za viungo wake mahiri Bastian Schweinsteiger, Thiago Alcantara na Javi Martínez, Lakini wadadisi wa masuala ya soka wanadai kuwa pengo la Alaba linaweza kuzibwa na Mbrazil Dante, Medhi Benatia au Jerome Boateng, Lakini pia wachezaji Philipp Lahm na Rafinha wote pia wanaweza kucheza nafasi hiyo.

Post a Comment

 
Top