Klabu ya Manchester
City imeiweka hadharani nia yake ya kutaka kupambana nje ya uwanja na klabu ya Bayern Munich kwenye mchakato wao wa malipo ya paundi milioni 20 kwa lengo la kuinasa saini ya kiungo wa Kijerumani anayekipiga kwenye klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani Marco Reus mwishoni mwa msimu huu.
Wakati kalabu yake ya sasa ya Borussia Dortmund ikiendelea kusisitiza kuwa Reus hataruhusiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo mnamo mwezi January lakini bado mchezaji huyo anaweza kuondoka kwenye dirisha hilo la usajiri kutokana na kipengele cha uvunjaji wa mkataba wake kuweka milango wazi kwa klabu yoyote itakayokua ikihitaji huduma zake kuweka mezani kiasi cha paundi milioni 20.
Mkataba wa sasa wa Reus mwenye umri wa miaka 25 unatarajiwa kukoma mnamo mwaka 2017 lakini kipengere hicho kinachoruhusu uvunjwaji wa mkataba huo ndio kinachoweka milango wazi kwa vilabu vyenye kuhitaji huduma zake kuweza kumyakua kiungo huyo mahiri.
Mabingwa wa ligi kuu nchini Ujerumani (Germay Bundesliga) klabu ya Bayern Munichen imeonesha nia ya kuwa tayari kulipa kiasi hicho cha pesa ili waweze kuzipata huduma za kiungo huyo lakini katika mbio hizo hawako pekeyao kwani klabu ya Manchester City nayo inavizia kwa ukaribu sana saini ya kiungo huyo ili kuendelea kuchanganya radha ndani ya kikosi chao.
Matajiri hao wa jiji la Manchester wamekuja na siraha kali zaidi ya kumshinda mpinzani wake kwani yenyewe tayari imekwishaanika hadharani kuwa mshahara rasmi wa kiungo huyo utakua ni Paundi laki mbili kwa wiki (200,000/=) wakiitumia kama chambo ya kumnasa kiungo huyo.
Liverpool na Manchester United nazo zimekua zikihusishwa sana na Reus, lakini inaaminika kuwa klabu ya Manchester City iko katika nafasi nzuri ya kumjumuisha Reus kwenye ligi ya masuperstar, mikiki na mishahara mikubwa ya Barclays
Premier League lakini pia tofauti kubwa ya kiushindani iliyopo baiana ya Bayern na Dortmund itakua ni chachu nyingine kwa wao kuweza kuipata saini ya mchezaji huyo.
Post a Comment