0
Yusuphu Mgwao mchezaji mpya wa Majimaji akitokea Friends Rangers ya jijini Dar es salaam.
KLABU ya Majimaji ya Mjini Songea leo ikiwa kwenye mji mdogo wa Makambako imekamilisha zoezi la upigaji picha zitakazo tumiwa na kampuni yenye haki ya urushaji wa matangzao ya Azam Tv kwaajili ya msimu mpya wa ligi.
Selemani Kibuta ametokea Mtibwa Sugar.
Akizungumza na mwandishi wetu aliyepo kwenye mji mdogo wa Makambako meneja wa timu hiyo Godfrey Ambrose Mvula amesema walikubaliana na wapiga picha wa kampuni hiyo kukutana kwenye mji huo ili kuwapunguzia safari ya kupanda na kushuka milima ya Lukumburu.
Paul John ametokea Polisi Moro.
"Tumekubaliana kukutana hapa na ndgugu zetu wa Azam ili tuwapunguzie safari ya kuja nyumbani kwetu Songea kwakua wana takiwa kuwahi mkoani Mbeya kwenda kukamilisha zoezi kama hilo kwa wenzetu walioko Mbeya pia na kama unavyoona siku zimetaradadi" Alisema Mvula.
Amani Simba
Aidha Mvula amesema wao kama klabu ya Majimaji tayari walishakua na makubaliano ya kuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya ligi daraja la kwanza ya Mji Njombe hivyo hata haikua tabu kwao kukubaliana na maombi ya wapiga picha wa Azam Tv kwakua walishakua na mpango wa kuelekea mjini Makambako.
Marcel Boniventure Kaheza "Rivaldo"
Akizungumzia mchezo huo wa kesho utakaochezwa kwenye uwanja wa Amani Makambako Mvula amesema watautumia mchezo huo kama kipimo chao cha mwisho kabisa kabla ya mchezo wao wa mwanzo wa ligi watakaocheza kwenye dimba la Majimaji mjini Songea dhidi ya klabu ya Tanzania Prison kutoka Jijini Mbeya.
Hamad Kibopile mashabiki wa Majimaji wamempachika jina la Evra kutokana na umahiri wake dimbani
"Tutautumia mchezo huu kukipa mazoezi ya mwishomwisho kabisa kikosi chetu ambacho kama unavyoona kina mabadiliko makubwa sana kwakua tumesajiri wachezaji wengi sana wageni kutoka kwenye vilabu mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania.

Iddi Kipangwile
Tumecheza michezo mingi sana ya kirafiki nyumbani na michezo miwili dhidi ya Mlale JKT ndio inabakia kuwa ni kipimo sahihi kwetu sisi kutokana na aina ya kikosi walichonacho na mashindano wanayoshiriki.
Fredy Mbuna ni mmoja wa wachezaji wanaounda kikosi cha Majimaji
Hivyo tumeona ni bora tuje tucheze dhidi ya timu ya mji Njombe kwani ni imani yetu kuwa ubora wao hautofautiani sana na ule walionao Mlale Fc hivyo nao pia watakua ni kipimo sahihi kwetu sisi." Alisema Mvula.
Bahati Yusuph aka Mwana Mbinga

Post a Comment

 
Top