0
Club ya Majimaji ya mjini songea leo itajitupa kwenye dimba lao la nyumbani la Majimaji kwaajili ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya vijana wa LIZABONI JR kutoka maeneo ya Lizaboni Songea.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu meneja wa kl;abu ya Majimaji Goddy Mvula amesema kua huo ni mwendelezo wa michezo ya kirafiki baada ya wikiendi iliyopita kukipiga dhidi ya Mlale Fc na kupata ushindi wa magoli 2:1.

"Klabu ya Lizaboni Jr ni moja kati ya timu ambazo zinashiriki mashindano mbalimbali hapa manispaa ya Songea lakini pia ni timu ambayo iko tayari muda wote unapoihitaji kuchezanayo mchezo wa kirafiki hivyo tumeonelea tucheze na wanalizaboni hawa ili angalau tuweze kuendelea kukipima kikosi chetu kwaajili ya ligi ijayo" Alisema Mvula.

Aidha Mvula amethibitisha kuwa timu hiyo siku ya jumaatatu itakua ikisafiri kuelekea mkoani Njombe ambako pamoja na kwenda kukamilisha zoezi la upigaji picha linalofanywa na Azam lakini pia wanatarajia kuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mji Njombe au Kombaini ya mjini makambako kwa kadri ambavyo mawasiliano yatakaa sawa na viongozi wa timu husika.

Timu  ya Majimaji imekua kwenye mazoezi ya nguvu ikijiandaa kwaajili ya msimu mpya wa ligi kuu wa mwaka 2016/2017

Post a Comment

 
Top