Kocha Hans van Pluijm leo atakuwa na kazi moja ya kurudisha
matumaini ya sana Yanga wakati atakapo kuongoza kikosi chake kucheza na
MO Bejaia ya Algeria.
Hiyo ni mechi ya mzunguko wa tano katika kundi A la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF.
Katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kikosi
cha Yanga kinachoshikilia nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo kitamkosa
mshambuliaji wake mahiri Donald Ngoma mwenye kadi mbili za njano.
Mbali na Ngoma pia kocha Pluijm yupo katika hatihati ya kuwapoteza
walinzi wake wawili wa kati Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kelvini Yondani
kutokana na majeruhi yanayo wakabili.
Nafasi hizo huenda zikazibwa na mabeki Vicent Bossou na Endrew Vicent
ambao wameonekana kufanya vizuri kwenye mazoezi ya kuiandaa na mchezo
huo wa kesho.
Pluijm amesema mchezo utakuwa mgumu kwasababu kila timu in a malengo
na mbinu zao za mchezo waliojifundisha hivyo anauhakika na matoke .
Pluijm amesema maandalizi yao kuelea mchezo huo wa leo yamekamilika
na kitu cha msingi kwao ni ushindi ili kufufua matumaini ya kucheza
nusu fainali.
"Tunawakaribisha nyumbani Bejaia, lakini wajiandae kwa kupiga kwani
ninaijua vizuri timu yao siyo nzuri wanacheza bila mpangilio na
tulipokuwa kwao tuliwazidi kwa kumiliki mpira na kuwashambulia sana
lakini walikuwa wakijiangusha na kupoteza muda," amesema Pluijm.
Mdachi huyo amesema kikosi chake cha kesho kinatarajiwa kuwa na
mabadiliko kidogo hasa baada ya Ngoma kukosekana kwenye mchezo huo.
Kwaupaunde wao MO Bejaia, wametamba kuendelea kipigo kwa wawakilishi
hao wa Tanzania kwasababu wananafasi nzuri nzuri ya kutinga nusu
fainali.
Nahodha wa timu hiyo amesema kwa kuzingatia hilo ndiyo sababu
wakaamua kuja mapema ili kuzoea hali ya hela lakini pia kupata muda wa
kutosha wa kupumzika kabla ya mchezo huo ambao K wao wameupa umuhimu wa
juu.
"Tunaiheshimu Yanga ni timu nzuri pamoja na kuwa nafasi ya mwisho
ndiyo maana tumekuja mapema kuhakikisha tunashinda mchezo huo kwasababu
tumejipanga vizuri na tunataka kucheza nusu fainali," amesema.
MO Bejaia ikishika nafasi ya tatu kwenye kundi A ikiwa na pointi 5
sawa na Medeama ya Ghana iliyopo nafasi ya pili lakini yenyewe ikiwa na
wastani mzuri wa mabao.
Post a Comment