0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linachukua nafasi hii kuipongeza Klabu ya Simba ya Dar es Salaam kwa kufikisha umri wa miaka 80 tangu kuanzishwa kwake kama ambavyo inaelezwa na viongozi wa sasa wa klabu hiyo.

Uongozi wa Simba SC kwa takribani miaka saba sasa, wamekuwa wakiazimisha siku ya Agosti 8, kila mwaka wamekuwa na wiki maalumu ya kuweka kumbukumbu ya kuanzishwa klabu hiyo ambako wanachama wao wanafahamu historia ya timu yao.


TFF tunasema kwamba hicho ni kitu kizuri, ambacho hakina budi kuenziwa kama ambavyo Simba hufanya kwa kushirikiana na jamii hasa kwa kufanya usafi katika mazingira mbalimbali, kutoa zawadi na kufanya ibada za kumbukumbu za waasisi wa klabu hiyo, wachezaji walioichezea Simba na kuipa mafanikio makubwa hususani kwa wale waliotangaulia mbele za haki.


Wito wetu ni kwamba Uongozi na wanachama wa Klabu ya Simba kuendeleze utamaduni huo wa kuadhikmisha wiki hadi siku ya Simba katika kuenzi historia ya klabu hiyo ambayo ina mchango wake mkubwa kwa soka la Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Chanzo: Simba damu fans blogspot

Post a Comment

 
Top