Salaam
Awali ya yote nimshukuru Mungu kwa kutujaalia uzima na uhai na pia kuendelea kuwasiliana ktk njia tofauti tofauti.
Pia niendelee kuwashukuru kwa sala na dua zenu kwangu binafsi zinazourejesha uoni wa macho yangu,ambayo nilikaribia kuyapoteza kabisa.
Ndugu zangu nimeamua kuja na ujumbe huu kwenu ukiwa na lengo kuu la kuendeleza umoja wetu ambao kwa sasa unahitajika kuliko kitu chochote na kuliko kipindi chochote kile.
Nyote mnafahamu hamu ya mwana Simba ni nini kwa sasa?
Mnafahamu pia,bila umoja madhubuti hatutaweza kufikia hamu na matarajio yetu ya uwanjani na nje ya uwanja.
Kwa maksudi kabisa nimeamua kuyaunganisha makundi yote ya Simba mitandaoni na nikianza na groups za Watsapp!
Na nimeona nianze na utaratibu ufuatao,ambao nnaamini sio tu utatupatia umoja,bali utarahisisha upatikanaji wa taarifa zote muhimu kuhusu Simba.
Kila group la Simba litaendelea na kanuni na taratibu zake ilizojiwekea ambazo bila shaka hazitaruhusu uvunjaji wa sheria za mitandao,katiba na sheria za nchi na pia zitazokazo fuata misingi na utamaduni wa klabu yetu.
Kila group litatoa maadmin wawili watakaokuwa ktk group moja.ambao litaitwa Simba headquarter.au kwa kifupi SIMBA HQ GROUP.
Group hili kuu litakuwa na viongozi wakuu wa klabu wa klabu na wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ambapo maadmin wa magruop ya Simba watapata kuelezea na kutoa maoni yao mbali mbali kuhusu club yao.
Maoni hayo bila shaka yatakuwa yametoka miongoni mwa wanachama wa magruop hayo.
Hapa nna hakika yale mengi tusiyoyajua tutakuwa tumeyapata moja kwa moja kutoka kwa washabiki na wapenzi wa klabu yetu.
Group hili la maadmin ndio litakaloratibu na kudhibiti habari za uzushi znazotungwa kila kukicha kuhusu klabu yetu.na litakuwa source mahsuus kwa klabu.
Group litatengenezewa kanuni zitakazofuatwa na wajumbe wote.
Magruop yote ya Simba yatateua yenyew maadmin wa kuja ktk Simba HQ bila kupangiwa.
Huu ni mwanzo tu ktk kuunganisha umoja huu muhimu wa Simba.na nimeona tuanzie mitandaoni kwenye watsapp ambapo tunaamini ujumbe hufika kwa haraka zaid na kwa watu wengi.
Bnafsi nishaanza kutembelea vyumba vya habari kuelezea dhana ya klabu ya umoja.na ntatembelea news room zote na pia ntekwenda matawini kuzungumza dhana hii na wanachama.
Moja ya jukumu la msemaji wa klabu ya Simba ni kuisemea katiba yetu.na katiba yetu ipo very clear kuhusu umoja..
Ntauimba umoja msimu mzima ujao ili tuweze kufikia malengo yetu tuliojiwekea.
Ktk kutimiza kiweledi Simba HQ tutakuwa tutawaalika viongozi na wadau mbali mbali wa taasisi tofaut tofauti ili kupata majawabu ya masuala mbali mbali yenye maslah na Simba.
Group hili litazinduliwa siku ya jpili hii tarehe 14-8-2016.
Kwa Yale magruop yatakayoafikiana na mpango huu yanapaswa kunitumia majina ya maadmin wa groups hizo na majina ya magruop kisha nithibitishe kwa kuniunga kwa muda.
Huu ni mchakato na naamin wengine hawataweza kuukamilisha weekend hii..tutaendelea kuwajumuisha hadi pale tutakapoona vinginevyo.
Naomba ujumbe huu ufike kwenye groups zote za watsapp za Simba.
Ni mimi Haji S Manara
Simba nguvu moja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment