Louis van Gaal amedai kuwa Manchester United
wameshawishiwa na vyombo vya habari huku akimponda Paul Scholes baada ya
klabu hiyo kushinda Jumamosi.
Hazijawa kampeni mbaya kwa Manchester United, lakini mambo si mazuri
sana hata hivyo. Wakiwa na pointi 24 katika mechi 12 Ligi Kuu ya
Uingereza, klabu hiyo inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi,
lakini pointi moja tu nyuma ya vinara wa ligi Manchester City.
Wakati akiwa hana taabu kama zinazomkabili mwenzake, Jose Mourinho,
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amekuwa akiandamwa na maneno
na kukosolewa kila kukicha.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni na BBC katika Uingereza, gwiji
wa Manchester United, Paul Scholes alibainisha kuwa hawezi kuishabikia
timu ya meneja wa sasa wala falsafa zake.
“Kuna mapungufu namna wachezaji wanavyojituma na ubunifu hakuna.
Inaonekana [Van Gaal] hataki wachezaji wanaopambana na kufunga magoli –
ni timu ambayo siwezi kufurahia kucheza. Mfumo wao si kama ule ambao
angeupenda Sir Alex Ferguson.”
Van Gaal si mtu wa kurudisha maneno, ingawa, baada ya ushindi wa 2-0
dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi, Mdachi huyo aliamua kujibu maoni
ya Scholes.
“Nilifurahi jinsi walivyocheza dhidi ya CSKA Moscow kwa sababu sina
budi kukubali kuwa mashabiki wana maoni yao binafsi lakini nadhani
walishawishiwa na Paul Scholes na yote ambayo vimeandika vyombo vya
habari, lakini wanapaswa kuchambua pia mchezo dhidi ya CSKA Moscow.”
Mashabiki wa Manchester United wamerizika sana tunapokwenda kwenye
mapumziko ya kimataifa, pia baada ya klabu yao kushinda mechi ya Ligi ya
Mabingwa katikati ya wiki. Mashetani Wekundu hawajafungwa katika mechi
tatu za mwisho za michuano yote na watakuwa mapumzikoni hadi Novemba 21,
ambapo watasafiri kuikabili Watford Ligi Kuu ya Uingereza.
Post a Comment