0
Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa kiungo wake Muargentina Javier Mascherano hakupata maumivu makubwa kwenye paja lake kwenye mchezo wake dhidi ya Real Madrid hapo jana.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina aligongana na James Rodriguez mnamo kipindi cha kwanza ambao klabu yake ya Barcelona ilipata ushindi wa jumla ya magoli 4-0 kwenye dimba la Santiago Bernabeu na nafasi yake kuchukuliwa na Jeremy Mathieu dakika ya 27 tu ya mchezo.

Mascherano anabakia kwenye hati hati kushiriki mchezo wa UEFA Champions League siku ya Jumanne dhidi ya AS ROMA na mchezo wa Spanish La Liga dhidi ya Real Sociedad jumaamosi ijayo lakini klabu imesema lolote laweza kutokea.

Post a Comment

 
Top