Klabu ya Manchester United imefungua mazungumzo na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa yenye nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic.
Imefahamika kwamba klabu ya Manchester United wanamapungufu katika sehemu ya ushambuliaji na meneja Louis van Gaal anatarajiwa kumsajili mshambuliaji mpya ili kutatua tatizo lililopo ndani ya timu hiyo kwa sasa.
Majina ya washambuliaji kadhaa yamekua yakitajwa na kuhusishwa kujiunga na mashetani wekundu hao lakini taarifa zinadai kuwa mabingwa hao wa kihistoria wa ligi kuu nchini Uingereza wanataka kumpa kipaumbele mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake unatarajiwa kuisha itakapofika mwezi juni mwakani.
Post a Comment