Tottenham iko kwenye mazungumzo na mawakala wa mshambuliaji wa klabu ya Corinthians ya nchini Brazil Alexandre Pato.
Bosi wa klabu ya Tottenham Spurs Mauricio Pochettino anataka kumjumuisha kikosini mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan litakapofunguliwa dirisha la usajili la mwezi Januari mwakani.
Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo wa nchini Brazil ni kuwa mawakala wawili Giuliano Bertolucci na Kia Joorabchian, ambao wote ni mawakala wa Pato, wako jijini London kwaajili ya mazungumzo na mabosi wa klabu ya Spurs.
klabu ya Corinthians inahitaji kiasi cha paundi milioni 15 za uingereza ili kumuuza Pato ambaye takribani misimu yake miwili iliyopita aliitumikia kwa mkopo klabu ya Sao Paulo ya hukohuko nchini Brazil.
Pamoja na Spurs,lakini pia vilabu vya West Ham, Borussia Dortmund na Barcelona vyote vimeonesha nia ya kuzihitaji huduma za mshambuliaji huyo.
Post a Comment