Mshambuliaji superstar wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar amerejea kutoka kwenye kifungo chake na sasa yuko tayari kuwavaa wajeruhiwa Argentina siku ya Alhamisi kwenye mchezo wa kufuzu kwa kombe la Dunia kwa bara la Amerika ya kusini.
Neymar alikosa michezo miwili ya timu yake ya taifa ya Brazil ilipoambulia kichapo cha jumla ya magoli 2:0 dhidi ya Chile mwezi uliopita na ule ambao timu yake hiyo ilijinyakulia ushindi wa magoli 3:1 dhidi Venezuela kufuatia kutumikia adhabu yake aliyoipata mnamo mwezi June mwaka huu kwenye michuano ya Copa Amerika.
Post a Comment