Michuano ya soka ya timu za mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inaanza Jumamosi jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Burundi watafungua mashindano hayo kuanzia saa nane mchana saa za
Afrika Mashariki dhidi ya Zanzibar huku wenyeji Ethiopia wakimenyana na
Rwanda.
Mabingwa watetezi wa taji hili ni Harambee Stars ya Kenya ambao wataanza kutetea taji lao dhidi ya Uganda siku ya Jumapili.
Mchuano mwingine wa Jumapili utakuwa kati ya Somalia na Kilimanjaro Stars ya Tanzania bara.
Malawi imealikwa katika mashindano haya na itaanza michuano hii dhidi ya Sudan siku ya Jumatatu.
Kundi A
Ethiopia, Rwanda, Tanzania na Somalia
Kundi B
Burundi, Kenya, Uganda na Zanzibar
Kundi C
Djibouti, Malawi, Sudan Kusini na Sudan
Post a Comment