Kocha wa Yanga Mholanzi Hans van der Pluijm, amesema pamoja na
kuwa na safu kali ya ushambuliaji lakini anahitaji kuongeza
mshambuliaji mwingine.
Mshambuliaji atakayesaidiana na waliopo kwa ajili ya kufanya vizuri
kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakayo shiriki mapema 2016.
Pluijm amesema anaridhishwa na uwajibikaji wa washambuliaji
waliopo lakini anahitaji kupata mtu mpambanaji kwa ajili ya kuwasaidia
kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika lakini itategemea uwajibikaji wake
uwanjani na rekodi yake kutoka timu anayoichezea hivi sasa.
“Awali nilisema hatuta sajili lakini nimeamua kubadili mawazo nataka
kuongeza mshambuliaji mmoja kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo lengo
langu nikuwa na mtu mpambanaji ambaye atakuja bila kufanyiwa majaribio
kutokana na utayari wake,”amesema Pluijm.
Mholanzi huyo amesema mfumo wa usajili anaotaka kuutumia kumpata
mshambuliaji huyo ni yule atakayefanya mazoezi na timu siku mbili na
siku inayofuata anaingia uwanjani kwa ajili ya kufanya kazi bila kujali
ni michuano gani iwe ya ligi ya Vodacom au FA.
Kwa sasa Yanga ina washambuliaji wanne wenye uwezo mkubwa ambao ni
Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, Amissi Tambwe kutoka Burundi na wazawa
Malimi Busungu, Matheo Simon na Simon Msuva aliyekuwa mfungaji bora na
mchezaji bora msimu uliopita
Post a Comment