0
Ligi kuu ya nchini Uingereza Premier League imeigia kwenye wiki yake ya 13 huku nyasi za viwanja kadhaa zikiendelea kuumia kwa miamba kadhaa kushuka ugani kutafuta alama tatu muhimu.

Wachezaji wawili wa klabu ya Everton Ross Barkley na Romelu Lukaku wameendeleza moto wao wa kuzifumania nyavu mara baada ya kuisaidia timu yao kupata ushindi mnono wa jumla ya magoli 4:0 dhidi ya  Aston Villa, Wakati  Harry Kane ameendelea kubakia kuwa muhimili wa upachikaji mabao kwa klabu yake ya mara baada ya kuingoza vyema timu yake hiyo kupata ushindi mnono wa magoli 4-1 kwenye mchezo wa dabi ya jiji la London dhidi ya wapinzani wao wa mji mmoja West Ham United.

Viungo wa Kibrazil wanaokipiga kwenye klabu ya Liverpool Philippe Coutinho na Roberto Firmino nao wameendelea kung'ara mara baada ya kuiongoza vyema timu yao ya Liverpool kupata ushindi wa jumla ya magoli 4-1 dhidi ya vigogo wa ligi hiyo klabu ya matajiri wa jiji la Manchester Manchester City 4-1 kwenye mchezo ambao mlinzi wa liverpool Martin Skrtel alionesha uwezo mkubwa sana.

Wafuatao ni wachezaji ambao mtandao huu imewaona kuwa wamefanya vizuri sana katika timu zao na nafasi zao katika michezo ya juma hili lililokwisha.

1. MLINDAMLANGO.   (COSTER PANTILIMON-SUNDERLAND)


Mlinda mlango huyu raia wa Romania anayekipiga kwenye klabu ya Sunderland aliweza kufanya mambo makubwa sana katika mchezo dhidi ya Crystal Palace ambapo aliokoa michomo takribani saba ya wazi dhidi ya vijana wa Alan Pardew kwenye dimba la Selhurst Park.

2. WALINZI.

Seamus Coleman (Everton)




Toby Alderweireld (Tottenham)



Martin Skrtel (Liverpool)



Erik Pieters (Stoke City)


3. VIUNGO.

Philippe Coutinho (Liverpool)


Ross Barkley (Everton)


Andre Ayew (Swansea City)



4. WASHAMBULIAJI

Roberto Firmino (Liverpool)



Harry Kane (Tottenham)


Romelu Lukaku (Everton)



5. KOCHA.

Jurgen Klopp (Liverpool)


 6. MFUMO.

        (4-3-3)

Post a Comment

 
Top