Taifa Stars imepoteza mechi yake ya kirafiki ya
mazoezi dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 kwa kufungwa
mabao 2-0.
Mechi hiyo imechezwa kwenye Uwanja wa Eldorado nje kidogo ya jiji la
Johanesburg na muda mwingi vijana hao wanaofundishwa na Shau Bartlet
aliyewahi kuchezea Charlton Athletic ya England na Bafana Bafana
walitawala zaidi kipindi cha kwanza kwa kiasi kikubwa.
Baada ya mechi hiyo, Kocha Charles Boniface Mkwasa alisema wachezaji wake walicheza kwa tahadhari kubwa kwa hofu ya kuumia.
"Lakini kikubwa lilikuwa ni suala la mazoezi na kuangalia makosa ni
nini na kipi cha kurekebisha," alisema Mkwasa alipokuwa akihojiwa na
Saleh Ally.
Baada ya mechi hiyo ya jana, Stars imemaliza rasmi kambi yake ya Afrika Kusini na leo inaanza safari kurejea nyumbani.
Kikosi cha Kikosi kilikachoanza mechi ya kirafiki:
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Haji Mwinyi
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani
6. Jonas Mkude/Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Salum Abubabary/Frank Domayo
9. John Bocco/Elius Maguri
10.Mrisho Ngassa/Malimi Busungu
11. Farid Mussa/Salum Telela
Post a Comment