0
Neymar jana alifunga magoli mawili kati ya matatu ambayo klabu ya Barcelona waliifunga klabu ya Villarreal na moja kati ya magoli hayo likitajwa kuwa ni miongoni mwa magoli bora kabisa kuwahi kufungwa na mshambuliaji huyo raia wa Brazil tangu atue kwenye klabu hiyo.


Magoli hayo yamekuja wakati mashabiki wa Camp Nou wakiwa bado wanalitaja jina la mfalme wao wa mabao Leo Messi ambaye hakuwemo kwenye kikosi hicho akiwa bado anauguza majeraha yake yanayomsibu.


Kiwango cha hali ya juu kilichooneshwa na Mbrazil huyo hapo jana kimezusha mjadala mzito miongoni mwa wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya soka ulimwenguni juu ya umuhimu wa Messi kwenye kikosi hicho.



Wachambuzi wengi wamemwagia sifa mshambuliaji huyo kwa kudai kuwa kutokana na uwezo huo uliooneshwa na mshambuliaji huyo ni wazi kuwa Barca sasa iko tayari kutua ugani pasi na Messi kuwepo na timu hiyo ikapata ushindi wa kishindo lakini pia kuwapa burudani wapenzi wake.



Post a Comment

 
Top