0

KOCHA wa Real Madrid Mhispania Raphael Benitez amekiri kuwa 'alichemka' kutompanga hata kiungo mmoja wa asili wa ukabaji.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Hispania, La Liga ambapo timu yake ilibugizwa mabao 4-0 na Barcelona, Benitez alisema alipanga viungo watatu Luka Modric, Toni Kroos na James Rodriguez ambao wote kiasili ni viungo washambuliaji kwa lengo la kutaka kumiliki mpira, kuwapa presha Barcelona kwa kuwashambulia sana ili kupata mabao mengi.

 
"Tulipanga BBC (Benzema, Bale na Christiano) huku nyuma yao kukiwa na viungo washambuliaji watatu kwa lengo la kuwashambulia kwa kasi wapinzani wetu na kuwapa presha ya juu". Alisema Benitez.

 
Benitez ambaye kabla ya mechi hii kulikuwa na tetesi kuwa atafukuzwa kwa kupoteza mchezo huu, alieleza kuwa mpango wao huo ulifeli kwavile walikutana na timu (Barcelona) ambayo ilikuwa bora sana na kukiri kuwa alimhitaji Casemiro ambaye ni kiungo mkabaji asilia.

 
"Tumeshindwa kufanikisha mipango yetu kwavile ilivurugwa na timu bora sana, ila kama tungefanikiwa basi leo tungeibuka na ushindi mnono". Alisisitiza Benitez.


Baada ya matokeo hayo mabaya, kocha huyu aliyekulia klabuni hapo akiwa kinda alisema kwasasa anajipanga kuirudisha timu pamoja kisaikolojia ili kushinda mchezo ujao.

 

Post a Comment

 
Top