Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania bara ‘Kili Stars’, Abdallah
Kibadeni amesema pamoja na kushinda mechi mbili zilizopita za kundi A,
lakini wanataka kuwafunga na wenyeji Ethiopia watakapocheza nao Jumamosi
kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Ethiopia.
Kibadeni amesema wanataka kurudisha heshima ya Tanzania hivyo
ni lazima kushinda kila mchezo licha ya kwamba tayari wamepata nafasi
ya kucheza robo fainali.
“Itakuwa mechi ngumu zaidi kwa kuwa tunakutana na wenyeji. Lakini
lazima tushinde na tumepania kufanya hivyo hatuna hofu na tunaamini sisi
ni bora kuliko wao na kushinda mechi zote za makundi kunafaida na
heshima yake,”amesema Kibadeni.
Kili Stars imecheza mechi mbili za michuano ya Chalenji ikianza kwa
kuifunga Somalia kwa mabao 4-0 kabla ya kuitoa nishai Rwanda kwa mabao
2-1 katika mechi ya pili.
Post a Comment