Kilimanjaro Stars ambayo ipo chini Abdallah Kibadeni
imefuzu hatua ya robo fainali Cecafa baada ya kuinyamazisha Rwanda kwa
kuichapa kwa mabao 2-1.
Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Wassa, Stars ilipata bao moja katika kila kipindi.
Bao la kwanza liliwekwa kimiyani na Said Ndemla na la pili likatupiwa
na Simon Msuva katika kipindi cha pili baada ya kipa wa Rwanda kufanya
uzembe.
Stars imefikisha ponti sita baada ya kuifunga Somalia kwa mabao 4-0
katika mechi ya kwanza pamoja na ushindi wa Jumanne dhidi ya Rwanda.
Tayari Kilimanjaro Stars wamejihakikishia nafasi ya kufuzu hatua
nyingine ya michuano hiyo inayoendelea Ethiopia, kwani hata timu
nyingine katika kundi lake itafikisha pointi 6, kuna faida nyingine ya
magoli mengi ya kufunga.
Mechi ya mwisho ya Kili Stars hatua ya makundi itakuwa dhidi ya
wenyeji Ethiopia walioanza michuano kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa
Rwanda.
Rwanda amabyo ilipata ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya
wenyeji Ethiopia, inashika nafasi ya pili huku Ethiopia wakishika nafasi
ya tatu na Somalia nafasi ya nne.
Katika mechi ya awali, Zanzibar Heroes ilitandikwa mabao 4-0 Uganda
ambao walianza michuano hiyo kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Kenya.
Siku ya Jumatano, Malawi itamenyana na Djibouti huku Sudan Kusini ikicheza na jirani yake Sudan.
Mchuano mwingine Somalia watamenyana na Ethiopia huku mabingwa watetezi Kenya wakimenyana na Burundi.
Post a Comment