Nahodha wa zamani wa klaby ya Livepool, Steven Gerrard anatarajiwa kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamni kwaajili ya mazoezi wiki ijayo. Kiungo huyo anatarajiwa kuwa chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Juergen Klopp.
Gerrard, anayekipiga kwenye ligi kuu ya nchini Marekani kwenye klabu ya LA Galaxy amekutana na kocha Klopp
mapema mwezi huu na Mjerumani huyo alimwalika nahodha huyo wa zamani kwenda kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha klabu hiyo katika kipindi hiki cha mapumziko cha ligi kuu ya mpira wa miguu ya nchini Marekani (MLS).
"Ninatarajia kujiunga na liverpool kwaajili ya mazoezi wiki ijayo na ninatarajia kuwepo pale kwa wiki kadhaa na nitakua chini ya mwalimu Klopp".
Post a Comment