ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola,
amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha timu ya Geita Gold SC
inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
Baada ya kusaini mkataba huo Matola amesema anajisikia furaha
kukamilisha mpango huo na hicho kitakuwa ni kipimo kizuri kuonyesha uwezo
wake kama kocha mkubwa anayeweza kufundisha timu kubwa Afrika.
“Nilipata ofa nyingi kabla ya kuja Geita lakini niliweza kuangalia
sera za timu zinakwenda vipi, baada ya kuongea na uongozi wa Geita hasa
mwenyekiti Bw. Salum kiukweli niliona ni watu wenye mwelekeo sasa nipo
tayari kuonyesha uwezo wangu halisi kama kocha mkuu wa Geita,” amesema
Matola.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Geita Bw. Salumu
Kulunge amesema wameamua kumtafuta Matola kwasababu anauwezo mkubwa wa
kazi hiyo na wanaamini ataipandisha timu hiyo kucheza ligi ya Vodacom
msimu ujao.
Mtihana mkubwa uliopo mbele ya Matola ni kuhakikisha timu hiyo
inapanda daraja kucheza Ligi ya Vodacom msimu ujao, baada ya kujaribu
mara kadhaa na kushindwa.
Post a Comment