KATIBU mkuu wa klabu ya The Might Elephant ya mkoani Ruvuma inayoshiriki ligi daraja la pili amesema kwamba wamekubaliana na shirikisho la Soka nchini Tanzania (Tff) kuwa fedha ambazo wanadai za mashindano ya kombe la FA, The Might Elephant watakatwa Juu kwa juu na kitachobaki basi watalipwa.
Akizungumza na Kipindi cha michezo leo cha Jogoo fm ya mjini Songea Katibu Chang'walu amesema kuwa wao kama timu wamekubaliana na TFF na hawana shida tena ya kuwadai badala yake watakatana juu kwa juu katika gharama mbali mbali ambazo The Might elephant itakutana nazo katika ligi ijayo ikiwemo uendeshaji wa ligi,leseni za wachezaji na gharama nyingine na Pesa itayobaki watalipwa.
"Pesa bado hawajatupa lakini tumekaa chini na tumefikia makubaliano kwamba kuna gharama za ushiriki pamoja na gharama za leseni za wachezaji ukijumlisha gharama za ushiriki ni sh.laki mbili,na gharama za leseni za wachezaji ni sh.laki tatu wachezaji thelathini, jumla yake ni sh.laki tano sasa katika makubaliano tuliyofikia ni kwamba sababu wao hawana fedha katika Kipindi hiki basi gharama hizo zikatwe katika fedha zetu tunazowadai ambapo sasa zitabakia sh.million mbili tu"Alisema Katibu Chang'walu.
Aidha Katibu amesema kuwa Tff wamewaandikia barua ya kuthibitisha hilo na wao kama The Might Elephant tayari wameshalipeleka kwa uongozi wao wa juu ambapo kwa sasa lipo kwa Mlezi Afande Luteni Kanali Chausi ambaye ni mwenyekiti wa timu na likitoka hapo litakwenda kwa mlezi mkuu ambaye ni Afande Brigedi Kamanda.
Post a Comment