UONGOZI wa Klabu ya Majimaji ya mjini Songea umewataka
wanachama,Wadau na Wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Siku ya Jumatano
katika uwanja wa Majimaji uliopo katikati ya mji kwa ajili ya mkutano wa
kujadiliana mambo kadha wa kadha.
Akiongea na Onesmo Emeran katika Kipindi cha michezo cha
Jogoo fm ya Mjini Songea Afisa habari wa Majimaji Nathan Mtega amesema kuwa
mkutano huo Agenda zake ni Pamoja kujadili mustakabali wa Majimaji katika
kuelekea Msimu mpya wa 2016/2017 lakini pia kwa ajili ya kuwashirikisha wadau
mbalimbali wa Soka mkoani hapa juu ya timu yao kwani hii ni timu ya mkoa.
"Tuwaombe mashabiki,wapenzi na wanachama wa Majimaji
kujitokeza kwa wingi siku hiyo sababu tunataka kujadili mustakabali wa timu
yetu katika ushiriki wa ligi kuu Tanzania bara lakini pia kujibu maswali ambayo
wengi wamekuwa wakijiuliza na kujipa majibu wenyewe ikiwemo suala la Kocha
Kally Ongala Pamoja na Suala la Symbion.
Lakini nirudie kwa wadau kujitokeza kwa wingi ili
tujadili kwa pamoja kuhusiana na Mustakabali wa timu yetu kuhusu kambi,kuhusu
Usajili n.k na muda wake ni kuanzia saa kumi Kamili jioni na kuendelea Amesema
Mtega"
Aidha Mtega amewataka wadau kujitokeza kwa wingi sababu
mkutano huo haubagui na hauchagui kama una kadi au ni mwanachama hai au si hai
ilimradi tu uwe ni mdau wa Soka basi Milango iko wazi kwao katika kushiriki
katika mkutano huo.
Post a Comment