Klabu ya Simba imethibitisha kuvunja mkataba na mshambuliaji wake
hatari wa msimu uliopita Mganda Hamisi Kiiza, kwa sababu ambazo wanazijua
wenyewe na hawajaziweka wazi.
Rais wa Simba Evans Aveva, amesema wanamshukuru Kiiza kwa
mchango wake mkubwa alioutoa kwa timu yao msimu uliopita na wanamtakia
kila la heri huko anapokwenda.
“Tumemalizana naye kila kitu na hatuna deni naye wale yeye hatudai na
hayo ni maamuzi yetu ambayo tunadhani yatakuwa na msingi kwa faida ya
timu yetu,”amesema Aveva.
Kiiza alikuwa mfungaji bora wa timu hiyo katika mashindano yote
akifunga mabao 19, kwenye Ligi ya Vodacom lakini pia akafunga mabao 5
kwenye michuano ya Kombe la FA.
Wapenzi, wanachama na mashabiki wa mpira wa miguu wamekua na maoni tofauti juu ya kitendo cha uongozi wa klabu ya Simba kuamua kuachana na mshambuliaji huyo.
Suala kubwa wanalolisimamia wanachama hao na mashabiki ni kitendo cha uongozi huo kutokujifunza jambo kutoka kwa Amisi tmbwe ambaye walimuachia na kuibukia kwa watani wao wa jadi Yanga.
Wakati Simba wanamuachia Tambwe alikua ndio Mfungaji bora wa ligi na mara baada ya kutimkia Jangwani amewasuta viongozi hao baada ya kuendele vyema na kazi yake ya ufungaji mpaka kuibuka kuwa mfungaji bora wa ligi wa msimu uliopita.
Swali la msingi linalogonga vichwani mwa wadadisi wa masuala ya soka ni hatua hiyo ni sahihi au sio sahihi?
Post a Comment