0
Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha dili la kumsajili winga Shizza kichuya kutoka Mtibwa Sugar kwa dau la milioni 20 na kumpa mkataba wa miaka miwili.


Katibu Mkuu wa Simba Patrick Kahemela, na afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar Thobiasi Kifaru wote kwa nyakati tofauti wamethibitisha juu ya uhamisho huo wa winga huyo mwenye kasi awapo dimbani.

Kahemele amedai kuwa tayari wamemalizana na uongozi wa Mtibwa na mchezaji huyo kwa sasa ni mali yao na atakuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachokwenda Morogoro kupiga kambi kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi Agasti.


“Tayari tumekamilisha dili la kumuuza Kichuya, kwa hiyo ameshajiunga na wenzake wa Simba, ni mchezaji mzuri ambaye tulikuwa tukitamani kuwa naye siku nyingi tukiamini anaweza kutupa mafanikio msimu ujao,”amesema Kifaru alipokua akiongea na Mwandishi wa habari za michezo wa kituo cha redio Jogoo Fm cha mjini Songea Onesmo Emeran.


Aidha Kahemele amesema wakati wanaendelea na kambi wataendelea kusajili wachezaji wapya ambao wataanza majaribio kupitia mazoezi yao ya jijini.

Post a Comment

 
Top