0
Nahodha wa klabu ya Simba Hassan Isihaka, amejiunga na Ndanda FC ya Mtwara kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kutokuwa kwenye mipango ya kocha mpya wa timu ya Simba Joseph Omog.

Isihaka amesema anajisikia furaha kutua Ndanda FC, kwasababu anaamini ni moja ya timu kubwa na yenye malengo mazuri katika Ligi ya Vodacom na atajitahidi kutumia uwezo wake kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi ya msimu ujao.

“Watu wanaweza kujiuliza nimetoka timu kubwa na kwenda timu ndigo Ndanda siyo timu ndogo kama wanavyodhani ndiyo maana inashiriki ligi ya Vodacaom kama ilivyo Simba Yanga na Azam kama mchezaji wa timu hii nitajitahidi napambana kuipigania ili iweze kufanya vizuri msimu ujao,”amesema Isihaka.

Isihaka alivuliwa unahodha kwenye klabu ya Simba msimu uliopita baada ya kulumbana na kocha wa wakati huo Jackson Mayanga, baada ya kum kumgomea kuingia uwanjani katika mchezo wa hatua ya 16 bora katika michuano ya kombe la FA dhidi ya Singida United.

Isihaka alimuuliza Mayanja ‘Kwanini hakumtumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga na kumpanga mchezo huo dhidi ya timu ndogo ya daraja la kwanza ambapo Simba ilishinda kwa mabao 5-1 na hapo ndipo uhasama ukaanza na kusimamishwa kwa mwezi mmoja kwa kusa hilo.

Baada ya kumaliza azabu hiyo aliporudi alipoteza nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza na kuvuliwa unahodha huku Novatus Lufunga akiziba na kucheza vizuri kwenye nafasi hiyo.

Chanzo; Goal.com

Post a Comment

 
Top