Juma Nyumayo akichangia jambo kwenye kikao hicho. |
katika kile kinachoonekana kama ni mwanzo mbaya wa msimu kikao cha pamoja kilichoitishwa na uongozi wa klabu ya Majimaji Fc (Wanalizombe) kimemalizika hapo jana pasi na kufikiwa muafaka wowote baada ya mwenyekiti wa timu hiyo ndugu Humphuley Milanzi kuamua kukiahirisha kikao hicho ilhali wajumbe waliohudhuria kikao hicho wakiwa na hamu ya kutaka kujua mustakabali wa timu yao.
Katibu wa Majimaji Frank Mbano akisoma maadhimio ya kamati ya Utendaji. |
Dalili za kukosekana kwa amani kenye kikao hicho zilianza kujionesha tangu awali kutokana na wajumbe mbalimbali waliokua wakipewa nafasi ya kuchangia au kuomba muongozo wa mwenyekiti wa kikao kuonekana wakichangia kwa hisia kali na wakati mwingine jazba ya hali ya juu.
Mkufunzi wa chuo cha St.Augustine Willy Migodela akichangia jambo kwenye kikao hicho. |
Hali hiyo ilisababisha kutolewa kwenye meza kuu Diwani wa kata ya Misufini Ndugu Ismail Azizi ambaye alikua akiomba muongozo wa mara kwa mara kutoka kwa mwenyekiti au katibu walipokua wakitoa taarifa au ufafanuzi wa maswala mbalimbali waliyokua wakiulizwa na wajumbe waliokuwepo kwenye mkutano huo.
Diwani wa kata ya Misufini Ismail Azizi akichangia kutokea jukwaani mara baada ya kufurushwa kutoka meza kuu. |
Hali ya mambo ilionekana huchafuka zaidi mara baada ya mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma (FARU) ndugu Golden Sanga aliponyanyuka na kutoa ufafanuzi mrefu kidogo kuhusiana na hali ya mambo ilivyo ndani ya timu hiyo.
"Inabidi uongozi wa Majimaji uketi
na bodi yake uzungumze kwa undani zaidi juu ya madeni ambayo iko nayo
lakini pia lazime iangalie kwa haraka zaidi kuhusiana na usajili ili
kuinusuru timu isishuke daraja kwani timu hii ilipo sasa hivi si ya
kumsusia mtu ni ya kwetu sote." Alisema Sanga.
Kiungo wa zamani wa klabu ya Majimaji na wekundu wa msimbazi Simba Stephen Mapunda "Garincha" alikua ni mmoja kati ya waliopata wasaa wa kuchangia kwenye mkutano huo. |
Mara baada ya maelezo hayo ya mwenyekiti wa FARU katibu wa chama cha soka Wilaya ya Songea Mjini (SUFA) Godfrey Ambrose Mvula alisimama na kutoa muongozo mbele ya mkutano huo hali ambayo haikupokelewa vyeama na wanachama hao walioamua kuanza kuzomea.
"Naomba tuelewane hapa huyu Sanga ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma na ndio mmoja kati ya walezi wa timu ya majimaji kama ilivyo kwetu sisi SUFA sasa inshangaza anapoacha kuwakumbusha majukumu yao viongozi wa Majimaji kwenye vikao maalumu na badala yake ameamua kuja kuwachongea mbele ya wanachama hapa, huu sio uongozi haiwezekani usubiri wenzako waharibikiwe wewe ndio usimame na kuwasema kiongozi bora ni yule anayewaongoza vyema watu wake." Alisema Mvula.
Mohammed Kaunda maarufu Mohammed Mchele alikuwepo kwenye kikao hicho. |
Mara bada ya sintofahamu hiyo mwenyekiti wa klabu ya Majimaji aliamua kuuvunja mkutano huo hali iliyosababisha wajumbe hao kuanza kusomea kwa sauti za juu huku viongozi hao wakiwa wanaondoka.
Post a Comment