Mjerumani Leroy Sane anaonekana kukubali kutimkia Manchester City baada ya kuripotiwa kuwa amekubali vigezo binafsi.
Mshambuliaji huyo wa Schalke 04 ambaye alikuwa katika kikosi cha
Ujerumani cha Euro 2016, ametajwa mara nyingi kukaribia kutua katika
Ligi Kuu ya Uingereza miezi ya hivi karibuni.
Habari zinadai kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 amekubali
kujiunga na kikosi cha Pep Guardiola kwa mkataba wa miaka minne lakini
bado klabu haijatoa ofa rasmi.
Kwa mujibu wa Bild, City wanaandaa kitita cha paundi milioni 46.5 ambacho kinaaminika kuwa kiasi ambacho Schalke wanakihitaji.
Iwapo City wataamua kusubiri hadi msimu ujao, Sane atagharimu miamba
hao wa Manchester kiasi cha paundi milioni 31.3, lakini inaaminika
mchezaji huyo anatamani zaidi kujiunga na klabu hiyo ya Uingereza sasa.
Sane amefunga mabao tisa katika mechi 42 alizocheza Schalke katika michuano yote msimu uliopita.
Post a Comment