Rogasian Kaijage |
TOTO AFRICANS ya Mwanza "Wanakisha
Mapanda"Wameanza rasmi Program ya Kusaka Vipaji (Scouting)kwa ajili ya
kuwajumuisha katika kikosi cha Toto ambacho kinashiriki ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika uwanja wa CCM
Kirumba Jijini Mwanza wakati akiwafanyia Majaribio vijana hao wapatao sitini na
tano(65) Kocha mkuu wa Toto Africans Rogasian Kaijage amesema kati ya hao
vijana 65 anaowahitaji ni kumi na tano(15) pekee kwa ajili ya kuongeza nguvu
katika kikosi hicho.
Kaijage amesema kuwa majaribio hayo ni ya wiki moja
kuanzia jumatatu (Jana)mpaka kufikia jumamosi awe tayari ameshapata Cream ya
vijana 15 ambao wataongeza nguvu kwa wanakishamapanda.
"Mimi nimeamua kuja kuwasaidia Toto sababu mimi ni
mwalimu wa Mpira na vijana wanataka msaada sijali kama Toto wataweza kunilipa
gharama yangu lakini mimi nipo hapa kwa ajili ya kuwasaidia Vijana".
"Mimi kama mwalimu na hapa nipo Nyumbani kwangu na
katika msimu uliopita nilipaswa kuingia katikati ili kuinusuru timu isije
kushukua daraja na nilikuwa kama mshauri tu lakini sasa nipo Full na ndiyo
maana nimeamua kuwaita Vijana Tanzania Nzima waje kufanya majaribio na nipo nao
hapa mpaka jumamosi nafanya Scouting.
Nipo na Vijana kama sitini na tano hivi na
ninahitaji kuwapata Vijana kumi na tano pekee ili waungane na wale wengine
waliokuwepo Msimu uliopita."Alisema Kocha huyo Mpya wa Toto Africans
Rogasian kaijage.
Aidha Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake
Twiga Stars amesema anaamini kati ya vijana hao Sitini na tano atapata vijana
kumi na tano ambao watakuwa na uwezo mkubwa wa kucheza.
Lakini kuhusiana na John Tegete ambaye ndiye alikuwa
kocha wa Toto Africans katika msimu uliopita suala hilo limekuwa gumu kujibiwa
kama amefukuzwa au atakuwa Kocha msaidizi au itakuaje.
Post a Comment